VICOBA • VIKUNDI VYA AKIBA • MICROFINANCE

Simamia Kikundi au Taasisi yako
kwa Urahisi na Usalama

VisaMi ni jukwaa la VICOBA, vikundi vya akiba na mikopo, na taasisi za microfinance: simamia michango, mikopo, marejesho na ripoti mahali pamoja, popote ulipo.

VisaMi Financial Technology•VIcoba + SAving + MIcrofinance
Usalama wa data Inapatikana Simu Kazi bila mtandao Imetengenezwa Tanzania Miezi 3 bure (wateja wapya)
👥
Wanachama & Wateja
Wa kikundi au wa taasisi, mahali pamoja
💰
Michango & Marejesho
Rekodi michango, marejesho na risiti
🏦
Mikopo
Kikundi na taasisi: omba, idhinisha, lipa
📊
Ripoti
Ripoti za fedha za kikundi na za matawi

Chagua huduma inayokuhusu

VisaMi (VIcoba + SAving + MIcrofinance) ni jukwaa moja kwa VICOBA, vikundi vya akiba na mikopo, na taasisi za microfinance.

VICOBA & Vikundi

Kwa vikundi vya akiba na mikopo: wanachama, michango, mikopo, mikutano, faini na ripoti.

  • Sajili kikundi bure na ongeza wanachama
  • Rekodi michango na toa risiti
  • Omba, idhinisha na fuatilia mikopo
  • Rekodi michango, marejesho na mahudhurio bila mtandao

Microfinance

Kwa taasisi za mikopo zenye matawi na wafanyakazi: wateja, mikopo, dhamana, marejesho na ripoti za fedha.

  • Matawi na majukumu: msimamizi, meneja wa tawi, afisa mikopo, mhasibu wa kaunta (teller)
  • Idhini za watu wawili kwa shughuli nyeti
  • Hesabu za fedha na kumbukumbu za ukaguzi
  • Bidhaa za mikopo, dhamana na wadhamini

Kila Kitu Unahitaji

Mfumo kamili wa kusimamia shughuli zote za kikundi au taasisi yako katika sehemu moja rahisi na salama.

Wanachama & Wateja

Sajili wanachama wa kikundi au wateja wa taasisi, angalia historia yao, michango, mikopo na hali yao yote.

Jifunza zaidi

Michango, Hisa & Marejesho

Rekodi hisa, akiba, michango na marejesho ya mikopo. Chapisha risiti moja kwa moja kwenye simu.

Jifunza zaidi

Mikopo

Omba na idhinisha mikopo, hesabu riba kiotomatiki, fuatilia dhamana, marejesho na baki zilizobaki.

Jifunza zaidi

Mikutano

Panga mikutano, rekodi mahudhurio na matokeo. Fuatilia agenda na maamuzi ya kikundi.

Jifunza zaidi

Faini

Rekodi faini za wanachama waliokosea sheria za kikundi na fuatilia malipo yao kwa usahihi.

Jifunza zaidi

Ripoti

Ripoti za fedha, mikopo na michango kwa vikundi (PDF), na ripoti za matawi na hesabu za fedha kwa taasisi.

Jifunza zaidi

Matawi & Majukumu

Taasisi yenye matawi mengi: msimamizi, meneja wa tawi, afisa mikopo na teller, kila mmoja na kazi zake.

Jifunza zaidi

Bidhaa za Mikopo, Dhamana & Wadhamini

Weka bidhaa za mikopo zenye riba, muda na ada, pamoja na dhamana na wadhamini kwa kila bidhaa.

Jifunza zaidi

Kaunta & Kufunga Siku

Teller anapokea marejesho na kutoa mikopo; kila siku fedha zinahesabiwa na tofauti zinaidhinishwa.

Jifunza zaidi

Idhini za Watu Wawili & Ukaguzi

Shughuli nyeti zinahitaji msimamizi wa pili, na kila tendo linahifadhiwa kwenye kumbukumbu ya ukaguzi.

Jifunza zaidi

Madeni Yaliyochelewa & Hasara

Fuatilia mikopo iliyochelewa kulipwa na weka makadirio ya hasara kwa viwango vilivyowekwa.

Jifunza zaidi

Kazi Bila Mtandao Mpya

Rekodi michango, marejesho na mahudhurio bila mtandao; kazi zinatumwa zenyewe mtandao ukirudi, bila kurudiwa.

Jifunza zaidi

Marejesho ya Siku, Wiki au Mwezi Mpya

Mkopo wa kila siku (siku 26 kwa mwezi, bila Jumapili), wa kila wiki (wiki 4 kwa mwezi) au wa kila mwezi; ratiba na kiasi cha kila malipo vinahesabiwa kiotomatiki.

Jifunza zaidi

Usalama na Udhibiti Mpya

Kiasi na riba ya mkopo haviwezi kubadilishwa baada ya kuundwa, msimamizi mkuu anasimamia tu bila kuingilia fedha za kikundi, na kila tendo linaandikwa kwenye kumbukumbu.

Jifunza zaidi

Siku 90 Bure, Kisha Lipa kwa Siku

Wateja wapya wanapata siku 90 bure kwa vikundi na taasisi. Baada ya hapo unalipa kwa siku kulingana na kifurushi chako.

Angalia bei

Mtandao Ukikatika, Kazi Haisimami

Mweka hazina, mwenyekiti na katibu wanaweza kuendelea kurekodi michango, marejesho na mahudhurio hata bila mtandao. Kazi zinahifadhiwa kwenye simu na kutumwa zenyewe mtandao ukirudi.

1

Andaa simu ukiwa na mtandao

Fungua Kazi bila mtandao mara moja. Orodha ya wanachama, aina za michango na mikopo inahifadhiwa kwenye simu yako.

2

Rekodi mahali popote

Mtandao ukikatika, weka mchango, marejesho au mahudhurio. Kila kazi inaingia kwenye foleni ya kutuma.

3

Mtandao ukirudi, inatumwa yenyewe

Kazi zinatumwa kiotomatiki, mara moja tu kila moja, na risiti rasmi inatolewa na seva.

Kazi bila mtandaoHakuna mtandao
MchangoAsha J. · Hisa5,000 Inasubiri
MarejeshoJuma M. · Mkopo LN-01420,000 Inasubiri
MahudhurioMkutano wa wiki18/20 Inasubiri
Mfano wa jinsi foleni inavyoonekana

Michango

Mweka hazina anarekodi hisa, akiba na michango mingine bila mtandao.

Marejesho ya mikopo

Malipo ya mikopo yanarekodiwa shambani au sokoni, na baki inasasishwa yakitumwa.

Mahudhurio ya mkutano

Mwenyekiti au katibu anaweka waliohudhuria; faini ya kutokuja inawekwa na mfumo.

Hakuna kurudiwa

Kazi ikitumwa mara mbili kwa bahati mbaya, mfumo unaipokea mara moja tu.

Salama kwa kifaa

Ukitoka (Toka), data ya offline inafutwa. Kuna pia kitufe cha kufuta data ya kifaa.

Pia kwa Microfinance

Teller na afisa wa mikopo wanapokea marejesho na kurekodi ziara bila mtandao.

Mambo ya kujua: mikopo mipya, idhini na ripoti za mwisho hubaki mtandaoni kwa usalama. Kazi iliyokaa zaidi ya siku 3 inahitaji uthibitisho kabla ya kutumwa, na ya zaidi ya siku 30 haikubaliwi. Fanya maandalizi (hatua ya 1) kabla ya kwenda eneo lisilo na mtandao.

Anza kwa Hatua Chache

Anza kutumia VisaMi ndani ya dakika chache.

1

Sajili Kikundi Chako

Unda akaunti kwa dakika chache: jina la kikundi, aina ya kikundi (VICOBA, Kikundi Kidogo au Umoja), eneo na msimamizi.

2

Ongeza Wanachama

Sajili wanachama wote. Kila mwanachama anaweza kuingia na kuona taarifa zake mwenyewe.

3

Anza Kusimamia

Rekodi michango, idhinisha mikopo (VICOBA), panga mikutano na fuatilia fedha zote na ripoti kwa urahisi.

Kila Mtu Ana Nafasi Yake

Mfumo huu umejengwa kwa ajili ya kila mwanachama wa kikundi na kila mfanyakazi wa taasisi, na uwezo tofauti kwa kila jukumu.

Msimamizi wa Taasisi

Anasimamia taasisi nzima: matawi, watumiaji, hesabu za fedha na idhini kuu.

  • Simamia matawi, watumiaji na majukumu yao
  • Ongeza fedha taslimu kwa idhini ya msimamizi wa pili
  • Idhinisha kufuta mikopo na tofauti za kaunta (na msimamizi mwingine)
  • Idhinisha uhamisho wa fedha kwenda benki (na msimamizi mwingine)
  • Angalia hesabu za fedha na pakua ripoti kwa CSV
  • Pitia kumbukumbu za ukaguzi za kila tendo
Kwa muhtasari
MatawiAnasimamia yote
Idhini nyetiWatu wawili
RipotiTaasisi nzima
Kumbukumbu za ukaguziKila tendo

Meneja wa Tawi

Anasimamia tawi lake: wafanyakazi, mikopo na fedha za kaunta.

  • Idhinisha mikopo ndani ya kiwango alichowekewa
  • Idhinisha au kataa maombi ya kurudisha malipo kutoka kwa teller
  • Fuatilia madeni yaliyochelewa ya tawi lake
  • Angalia ripoti za tawi
  • Simamia afisa mikopo na teller wa tawi
Kwa muhtasari
MikopoNdani ya kiwango chake
Kurudisha malipoAnaidhinisha
RipotiZa tawi lake
WafanyakaziWa tawi lake

Afisa Mikopo

Anafanya kazi na wateja: usajili, maombi ya mikopo na ufuatiliaji wa marejesho.

  • Sajili wateja wapya
  • Andaa ombi la mkopo pamoja na dhamana na wadhamini
  • Fuatilia marejesho ya wateja wake
  • Angalia ratiba ya marejesho ya kila mkopo
Kwa muhtasari
WatejaAnasajili
Maombi ya mikopoAnaandaa
IdhiniMeneja au msimamizi
Fedha taslimuHashughuliki nazo

Teller (Kaunta)

Anashughulikia fedha taslimu za kaunta: marejesho, kutoa mikopo na kufunga siku.

  • Pokea marejesho ya wateja
  • Toa mkopo (ada inakatwa mwanzo)
  • Omba kurudisha malipo yaliyokosewa (meneja au msimamizi anaidhinisha)
  • Hesabu fedha taslimu na funga siku ya kaunta
Kwa muhtasari
MarejeshoAnapokea
Kutoa mkopoAnatoa
Kurudisha malipoAnaomba tu
Kufunga sikuAnahesabu fedha

Mwenyekiti wa Kikundi

Ana udhibiti kamili wa kikundi — anaona kila kitu na anaweza kuidhinisha maamuzi yote ya fedha.

  • Angalia na simamia wanachama wote
  • Idhinisha na kataa maombi ya mikopo
  • Toa ripoti kamili za fedha (PDF)
  • Weka na badilisha sheria za kikundi
  • Angalia historia ya michango yote
  • Simamia faini na adhabu
Muhtasari wa Kikundi
Wanachama24 watu
Mikopo Inayosubiri3 maombi
Akiba ya JumlaTZS 4,250,000
Mikopo IliyotolewaTZS 1,800,000
Faini ZilizolipwaTZS 45,000

Katibu wa Kikundi

Anashughulikia kumbukumbu za kikundi — anarekodi michango, mikutano na matukio yote ya kila siku.

  • Rekodi michango ya wanachama
  • Panga na rekodi mikutano
  • Chapisha risiti za malipo
  • Rekodi faini na adhabu
  • Angalia ripoti za msingi
  • Tuma arifa kwa wanachama
Shughuli za Leo
Michango Iliyolipwa12 watu
Hawajalipa5 watu
Mkutano UjaoIjumaa 10:00
Risiti Zilizochapishwa12 risiti
Faini Mpya2 faini

Mwanachama wa Kawaida

Anaona taarifa zake mwenyewe tu — michango yake, mikopo yake, na hali yake ya sasa ndani ya kikundi.

  • Angalia michango yako yote
  • Omba mkopo moja kwa moja
  • Angalia hali ya mkopo wako
  • Pakua risiti za malipo yako
  • Angalia mikutano iliyopita
  • Tazama baki yako ya akiba
Taarifa Zangu
Hisa ZanguTZS 180,000
Mkopo WanguTZS 300,000
Baki ya MkopoTZS 120,000
Faini ZanguTZS 0
Hali Yangu✓ Nzuri

Jifunze kutumia VisaMi

Soma mwongozo wa hatua kwa hatua, kisha angalia majibu ya maswali ya kawaida.

VisaMi ni nini?

VisaMi = VIcoba + SAving + MIcrofinance. Jina kamili ni VisaMi Financial Technology: jukwaa la kidijitali kutoka Moescience kwa VICOBA, vikundi vya akiba na mikopo, na taasisi za microfinance.

Nikiwa na kikundi, ninaanzaje?

Bonyeza “Sajili kikundi”, jaza taarifa za kikundi, kisha ongeza wanachama na uanze kurekodi michango na mikopo. Mwongozo unaeleza kila hatua.

VICOBA na Microfinance vinatofautianaje?

VICOBA ni kwa vikundi vinavyokopeshana na kuweka akiba kati ya wanachama wenyewe. Microfinance ni kwa taasisi inayotoa mikopo kwa wateja kupitia matawi na wafanyakazi wenye majukumu tofauti.

Taasisi ya mikopo inaanzaje kutumia VisaMi?

Taasisi huandaliwa na timu yetu: tunaweka jina rasmi la taasisi, matawi na wasimamizi wawili. Wasiliana nasi kwa WhatsApp au simu. Baada ya hapo wafanyakazi huingia kupitia kiungo cha “Wafanyakazi: Ingia”.

Wafanyakazi wa taasisi wanaingia wapi?

Kupitia ukurasa wa kuingia wa wafanyakazi wa microfinance (kitufe cha “Ingia (MFI)” juu ya ukurasa huu). Ni tofauti na kuingia kwa wanachama wa VICOBA.

VisaMi inafanya kazi bila mtandao?

Ndiyo. Mweka hazina anaweza kurekodi michango na marejesho ya mikopo, na mwenyekiti au katibu mahudhurio, hata mtandao ukikatika. Kazi zinahifadhiwa kwenye simu na kutumwa zenyewe mtandao ukirudi, mara moja tu kila moja. Ili ifanye kazi, fungua “Kazi bila mtandao” mara moja ukiwa na mtandao. Mikopo mipya, idhini na ripoti za mwisho hubaki mtandaoni kwa usalama.

Nini kinatokea kifurushi kikiisha?

Siku 90 za kwanza ni bure. Kikiisha, watumiaji wanaona ukurasa wa “Kifurushi kimeisha” na hawawezi kuendelea kufanya kazi hadi ulipe. Data yako haipotei. Ukilipa na kuwasiliana nasi, akaunti inafunguliwa tena.

Je, mikopo ya kila siku au kila wiki inawezekana?

Ndiyo. Unaweza kuchagua marejesho ya kila siku (siku 26 kwa mwezi, bila Jumapili), kila wiki (wiki 4 kwa mwezi) au kila mwezi. Mfumo unahesabu ratiba na kiasi cha kila malipo.

Nawezaje kupata msaada?

Piga au tuma WhatsApp kwa +255 768 139 301, au tuandikie moescience@proton.me.

Bei Rahisi na Wazi

Lipa kwa Siku, Kwa Kifurushi Chako

Bei zote zinahesabiwa kwa siku. Andika siku unazotaka kulipia (kima cha chini siku 7) na uone jumla papo hapo.

Miezi 3 BURE kwa wateja wapya — mara moja tu, kisha unalipa kwa siku
Basic
Vikundi vya akiba (saving) na Umoja/familia
TZS 200kwa siku
TZS 6,000 kwa mwezi (siku 30)
  • Wanachama bila kikomo
  • Michango na akiba, risiti za kuchapisha
  • Mikutano na mahudhurio
  • Ripoti za PDF
  • Mikopo ya kikundi (iko kwenye VICOBA)
Maarufu
VICOBA
Vikundi vya VICOBA vyenye mikopo
TZS 500kwa siku
TZS 15,000 kwa mwezi (siku 30)
  • Kila kitu cha Basic
  • Mikopo: idhini hatua 4, riba na marejesho
  • Dhamana na faini
  • Gawio na ripoti za mkutano mkuu (AGM)
  • Ripoti za kina za fedha

Kikokotoo cha bei (kwa siku)

Bei kwa siku (kwa tawi)TZS 200
Siku30
Jumla ya kulipaTZS 6,000
Omba huduma (jaza fomu)
Wateja wapya: siku 90 za kwanza ni bure (mara moja tu). Malipo ya jumla hapo juu yanaanza baada ya kipindi hicho.
Bei = bei ya mwezi ÷ 30 × siku. Baada ya kuwasiliana nasi utapewa maelekezo ya malipo.
Wasiliana Nasi

Tuko Tayari Kukusaidia

Una swali kuhusu kifurushi, usajili au kuhamisha data? Tuandikie au tupigie — tutakujibu haraka.

Jiunge Nasi

Anza na VisaMi

Vikundi hujisajili wenyewe na kuanza mara moja. Taasisi huandaliwa na timu yetu baada ya ombi. Miezi 3 bure kwa wateja wapya.

Unajisajili mwenyewe, ndani ya dakika chache
  • Jina na aina ya kikundi (VICOBA, Kikundi Kidogo au Umoja)
  • Simu ya kikundi na eneo (mkoa na wilaya)
  • Taarifa za msimamizi (mwenyekiti) atakayetumia akaunti
Sajili kikundi (miezi 3 bure)

Microfinance kwa Taasisi

Kwa taasisi za mikopo zenye matawi na wafanyakazi wenye majukumu tofauti: fedha, mikopo na ripoti zikiwa na udhibiti na ukaguzi.

  • Taasisi moja au zaidi, kila moja ikiwa na matawi yake
  • Majukumu: msimamizi, meneja wa tawi, afisa mikopo na teller
  • Bidhaa za mikopo: riba, muda, ada, dhamana na wadhamini
  • Marejesho ya kila siku, wiki, mwezi au kila siku kadhaa unazochagua
  • Teller anapokea marejesho na kutoa mikopo; kila siku fedha zinahesabiwa na tofauti zinaidhinishwa
  • Shughuli nyeti zinahitaji idhini ya mtu wa pili
  • Hesabu za fedha, ripoti za tawi na kumbukumbu za ukaguzi zisizobadilika
Wafanyakazi: Ingia Omba huduma

Kazi Bila Mtandao Mpya

Mtandao ukikatika, endelea kurekodi; kazi zinahifadhiwa kwenye simu na kutumwa zenyewe mtandao ukirudi.

Kwa vikundi (VICOBA)
  • Mweka hazina: michango na marejesho ya mikopo
  • Mwenyekiti au katibu: mahudhurio ya mikutano
  • Kazi zinatumwa kiotomatiki mtandao ukirudi, mara moja tu kila moja
  • Risiti rasmi inatolewa na seva wakati wa kutuma
  • Ukitoka (Toka), data ya offline kwenye simu inafutwa
Kwa taasisi (Microfinance)
  • Teller na afisa: orodha ya wadaiwa, malipo na ziara bila mtandao
  • Kazi za zaidi ya siku 3 zinasubiri idhini ya meneja

Mikopo mipya, idhini na ripoti za mwisho hubaki mtandaoni kwa usalama. Andaa simu ukiwa na mtandao kabla ya kwenda eneo lisilo na mtandao.

Anza Sasa Bure

Usalama na Udhibiti

Fedha za kikundi zinalindwa kwa utaratibu wazi, majukumu yaliyotenganishwa na kumbukumbu zisizofutika.

  • Kila hatua ya mkopo inafanywa na mtu tofauti; hakuna anayeidhinisha mkopo wake mwenyewe
  • Mkopo ukishaundwa: kiasi, riba na hali yake havibadilishwi; tarehe, madhumuni na maelezo tu
  • Msimamizi mkuu wa jukwaa anasimamia tu; haingizi michango, marejesho wala mikopo ya vikundi
  • Kumbukumbu za ukaguzi zinaandika nani alifanya nini na lini
  • Taasisi: shughuli nyeti zinahitaji msimamizi wa pili
  • Kazi bila mtandao inalindwa dhidi ya kurudiwa, na data ya kifaa inafutwa unapotoka
Soma mwongozo

Siku 90 Bure, Kisha Lipa kwa Siku

Kila kikundi au taasisi mpya inapata siku 90 za kwanza bila malipo, mara moja tu.

  • Baada ya siku 90 unalipa kwa siku kulingana na kifurushi (Basic, VICOBA au Microfinance kwa kila tawi)
  • Kifurushi kikiisha, ukurasa wa “Kifurushi kimeisha” unaonekana na data yako inabaki salama
  • Ukilipa na kuwasiliana nasi, akaunti inafunguliwa tena
Angalia bei

Usimamizi wa Wanachama

Simamia wanachama wote wa kikundi chako kwa urahisi — kuanzia usajili hadi historia kamili ya kila mwanachama.

Kwa vikundi (VICOBA)
  • Sajili wanachama wapya haraka
  • Angalia historia ya michango ya kila mtu
  • Fuatilia mikopo na baki za kila mwanachama
  • Weka picha na taarifa za kibinafsi
  • Toa ripoti ya mwanachama mmoja mmoja (PDF)
  • Simamia hali ya uanachama (hai/hayupo)
Kwa taasisi (microfinance)
  • Sajili wateja wa taasisi na uwape namba
  • Weka tawi na afisa mikopo wa kila mteja
  • Angalia mikopo, dhamana na marejesho ya kila mteja
Anza Sasa Bure

Michango & Hisa

Rekodi aina zote za michango — hisa, akiba, usajili — na chapisha risiti moja kwa moja kwenye simu yako.

Kwa vikundi (VICOBA)
  • Rekodi hisa za kila mkutano
  • Rekodi akiba za ziada
  • Chapisha risiti za malipo (PDF/Print)
  • Angalia jumla ya michango yote
  • Toa ripoti ya michango kwa kipindi
  • Angalia walipolipa na ambao hawajalipa
Kwa taasisi (microfinance)
  • Pokea marejesho ya mikopo kwenye kaunta (teller)
  • Malipo hugawanywa kwa utaratibu: adhabu, riba kisha mtaji
  • Malipo ya ziada yanalipa awamu zinazofuata
  • Kurudisha malipo kunahitaji idhini ya meneja au msimamizi
Anza Sasa Bure

Mfumo wa Mikopo

Simamia mikopo yote ya kikundi — kuanzia ombi hadi kulipa — kwa usahihi na uwazi mkubwa.

Kwa vikundi (VICOBA)
  • Omba mkopo moja kwa moja kwenye mfumo
  • Mwenyekiti anaidhinisha au anakataa
  • Hesabu riba kiotomatiki (rahisi au mchanganyiko)
  • Rekodi malipo ya mkopo kila wakati
  • Angalia baki na riba iliyobaki
  • Toa ripoti ya mikopo yote (PDF)
  • Marejesho ya kila siku (siku 26 kwa mwezi, bila Jumapili), kila wiki (wiki 4 kwa mwezi) au kila mwezi
  • Mkopo ukishatolewa, kiasi na riba havibadilishwi; tarehe, madhumuni na maelezo tu
Kwa taasisi (microfinance)
  • Bidhaa za mikopo zenye riba, muda na ada zake
  • Wadhamini na dhamana kwa kila bidhaa
  • Meneja wa tawi anaidhinisha mikopo ndani ya kiwango chake
  • Teller anatoa mkopo; ada inakatwa mwanzo
  • Marejesho ya kila siku, wiki, mwezi au kila siku kadhaa
  • Fuatilia madeni yaliyochelewa na makadirio ya hasara
Anza Sasa Bure

Usimamizi wa Mikutano

Panga, rekodi na fuatilia mikutano yote ya kikundi chako — mahudhurio, agenda na maamuzi yaliyofikiwa.

  • Panga tarehe na wakati wa mkutano
  • Rekodi mahudhurio ya kila mwanachama
  • Weka agenda na maelezo ya mkutano
  • Rekodi maamuzi yaliyofikiwa
  • Angalia historia ya mikutano yote
  • Toa ripoti ya mahudhurio (PDF)
Anza Sasa Bure

Usimamizi wa Faini

Rekodi na fuatilia faini za wanachama waliokosea sheria za kikundi — kwa uwazi na usahihi.

  • Rekodi faini kwa aina tofauti
  • Rekodi malipo ya faini
  • Angalia faini zilizolipwa na zinazodaiwa
  • Historia ya faini za kila mwanachama
  • Jumla ya faini zilizokusanywa
  • Toa ripoti ya faini (PDF)
Anza Sasa Bure

Ripoti za PDF

Tengeneza na pakua ripoti kamili za hali ya fedha ya kikundi chako — kwa wakati wowote unaotaka.

Kwa vikundi (VICOBA)
  • Ripoti ya michango yote
  • Ripoti ya mikopo na baki
  • Ripoti ya faini zilizokusanywa
  • Ripoti ya mahudhurio ya mikutano
  • Taarifa ya jumla ya fedha za kikundi
  • Ripoti za kila mwanachama kibinafsi
Kwa taasisi (microfinance)
  • Ripoti za tawi na za taasisi nzima
  • Hesabu za fedha na vitabu vya hesabu
  • Pakua ripoti kwa CSV (msimamizi tu)
  • Kumbukumbu za ukaguzi zisizobadilika
Anza Sasa Bure
Weka App Simu Yako Weka VisaMi kwenye simu yako