VisaMiVisaMiFinancial Technology

Mwongozo wa matumizi

VisaMi  •  VIcoba + SAving + MIcrofinance
VICOBA • Savings Groups • Microfinance

VICOBA & VikundiAkiba, hisa, mikopo, mikutano na marejesho. Soma mwongozo kamili →MicrofinanceWateja, mikopo, dhamana, marejesho na usimamizi wa matawi. Soma mwongozo kamili →

Kuanza haraka

VisaMi (VIcoba + SAving + MIcrofinance) ina sehemu mbili. Chagua ile inayokuhusu:

Wateja wa taasisi ya mikopo hawaingii wenyewe kwenye mfumo. Wanahudumiwa na wafanyakazi wa tawi.

VICOBA na vikundi vidogo

Kujisajili na kuingia

  1. Fungua ukurasa wa kuingia na ubonyeze Sajili hapa (kikundi kipya).
  2. Jaza taarifa za kikundi na za mtu anayeanzisha. Huyo anakuwa msimamizi wa kikundi.
  3. Ingia kwa nambari ya simu au barua pepe na nywila yako. Usimpe mtu nywila yako.

Majukumu ya kikundi

JukumuAnachofanya
MwenyekitiAnaidhinisha mikopo hatua ya mwisho na anasimamia kikundi.
Mweka hazinaAnarekodi michango na marejesho, anathibitisha maombi ya mikopo.
KatibuAnasimamia kumbukumbu na anapitisha maombi ya mikopo hatua ya pili.
MwanachamaAnaona michango yake, anaomba mkopo na kuangalia salio lake.

Michango

  1. Mweka hazina anafungua ukurasa wa michango.
  2. Anachagua mwanachama, aina ya mchango na kiasi.
  3. Anahifadhi, na mwanachama anaona mchango wake mara moja.

Mikopo kwa hatua nne

  1. Mwanachama anawasilisha ombi la mkopo (kiasi, muda, aina ya riba).
  2. Mweka hazina anathibitisha ombi.
  3. Katibu anapitisha ombi.
  4. Mwenyekiti anaidhinisha, na mkopo unatolewa.

Hakuna anayeweza kuidhinisha mkopo wake mwenyewe. Mkopo uliokataliwa haurudi kwenye hatua ya awali; ombi jipya linaundwa.

Marejesho, faini na ripoti

Microfinance: taasisi, matawi na wafanyakazi

Kuingia

  1. Bonyeza Ingia (MFI) kwenye ukurasa wa mwanzo au wa kuingia, au fungua /mf/login.php.
  2. Ingia kwa barua pepe na nywila ya muda uliyopewa na msimamizi wa taasisi.
  3. Mara ya kwanza, mfumo unakulazimisha kubadilisha nywila. Chagua ndefu na ya kipekee.
  4. Utaona dashibodi yenye kazi zinazokusubiri kulingana na jukumu lako.

Nani anafanya nini

JukumuMajukumu makuu
Msimamizi wa taasisiAnaongeza wafanyakazi na matawi, anaweka bidhaa za mikopo, anaidhinisha mikopo mikubwa, na anaamua maombi ya fedha, kutengua malipo na tofauti za till. Kila uamuzi mkubwa unahitaji msimamizi wa pili.
Meneja wa tawiAnaidhinisha mikopo hadi kikomo chake, anafunga siku, na anaona ripoti za tawi.
Afisa mikopoAnasajili wateja, anaunda maombi ya mikopo na kufuatilia wateja waliochelewa.
TellerAnatoa mikopo na kupokea marejesho. Ndiye pekee anayeshika fedha taslimu za mteja.

Kusajili mteja

  1. Afisa mikopo anafungua Wateja > Mteja mpya.
  2. Anaingiza jina, simu, namba ya kitambulisho na tawi.
  3. Anathibitisha KYC (utambulisho) baada ya kuona kitambulisho halisi. Mfumo hauthibitishi kiotomatiki.

Kutoka ombi hadi mkopo

  1. Ombi: afisa anafungua Maombi ya mikopo na kuunda ombi kwa bidhaa, kiasi na muda.
  2. Idhini: meneja anaidhinisha hadi kikomo chake; juu ya hapo msimamizi anaidhinisha.
  3. Utoaji: teller anafungua Utoaji wa mikopo na kutoa fedha. Ada ya bidhaa inakatwa mbele, na mteja anapokea kiasi baada ya ada.
  4. Marejesho: teller anafungua Pokea malipo. Malipo yanagawanywa: faini, riba kisha mtaji. Malipo ya ziada yanalipa awamu za mbele; kilichobaki kinakwenda kwenye salio la mteja.

Kosa la malipo

  1. Teller anaomba kutengua malipo kwa kutoa sababu.
  2. Meneja au msimamizi anaamua. Teller hawezi kuidhinisha ombi lake mwenyewe.
  3. Ikikubaliwa, malipo yanatenguliwa na vitabu vinarekebishwa; risiti inaonyesha "imetenguliwa".

Mwisho wa siku

  1. Meneja anafungua Fedha > Kufunga siku, anahesabu fedha taslimu za kasha na kuziandika.
  2. Zikitofautiana na vitabu, anaandika maelezo na anaweza kumchagua teller anayehusika. Tofauti inasubiri msimamizi mwingine.
  3. Msimamizi mwingine anaamua kwenye Fedha > Tofauti za till: upungufu unakwenda gharama ya taasisi, ziada inakwenda mapato.
  4. Baada ya kufunga, hakuna miamala mipya ya fedha kwa tawi hilo siku hiyo.

Fedha, ripoti na usalama

Msaada na usalama