VisaMi ni jukwaa la VICOBA, vikundi vya akiba na mikopo, na taasisi za microfinance: simamia michango, mikopo, marejesho na ripoti mahali pamoja, popote ulipo.
VisaMi (VIcoba + SAving + MIcrofinance) ni jukwaa moja kwa VICOBA, vikundi vya akiba na mikopo, na taasisi za microfinance.
Kwa vikundi vya akiba na mikopo: wanachama, michango, mikopo, mikutano, faini na ripoti.
Kwa taasisi za mikopo zenye matawi na wafanyakazi: wateja, mikopo, dhamana, marejesho na ripoti za fedha.
Mfumo kamili wa kusimamia shughuli zote za kikundi au taasisi yako katika sehemu moja rahisi na salama.
Sajili wanachama wa kikundi au wateja wa taasisi, angalia historia yao, michango, mikopo na hali yao yote.
Jifunza zaidiRekodi hisa, akiba, michango na marejesho ya mikopo. Chapisha risiti moja kwa moja kwenye simu.
Jifunza zaidiOmba na idhinisha mikopo, hesabu riba kiotomatiki, fuatilia dhamana, marejesho na baki zilizobaki.
Jifunza zaidiPanga mikutano, rekodi mahudhurio na matokeo. Fuatilia agenda na maamuzi ya kikundi.
Jifunza zaidiRekodi faini za wanachama waliokosea sheria za kikundi na fuatilia malipo yao kwa usahihi.
Jifunza zaidiRipoti za fedha, mikopo na michango kwa vikundi (PDF), na ripoti za matawi na hesabu za fedha kwa taasisi.
Jifunza zaidiTaasisi yenye matawi mengi: msimamizi, meneja wa tawi, afisa mikopo na teller, kila mmoja na kazi zake.
Jifunza zaidiWeka bidhaa za mikopo zenye riba, muda na ada, pamoja na dhamana na wadhamini kwa kila bidhaa.
Jifunza zaidiTeller anapokea marejesho na kutoa mikopo; kila siku fedha zinahesabiwa na tofauti zinaidhinishwa.
Jifunza zaidiShughuli nyeti zinahitaji msimamizi wa pili, na kila tendo linahifadhiwa kwenye kumbukumbu ya ukaguzi.
Jifunza zaidiFuatilia mikopo iliyochelewa kulipwa na weka makadirio ya hasara kwa viwango vilivyowekwa.
Jifunza zaidiRekodi michango, marejesho na mahudhurio bila mtandao; kazi zinatumwa zenyewe mtandao ukirudi, bila kurudiwa.
Jifunza zaidiMkopo wa kila siku (siku 26 kwa mwezi, bila Jumapili), wa kila wiki (wiki 4 kwa mwezi) au wa kila mwezi; ratiba na kiasi cha kila malipo vinahesabiwa kiotomatiki.
Jifunza zaidiKiasi na riba ya mkopo haviwezi kubadilishwa baada ya kuundwa, msimamizi mkuu anasimamia tu bila kuingilia fedha za kikundi, na kila tendo linaandikwa kwenye kumbukumbu.
Jifunza zaidiWateja wapya wanapata siku 90 bure kwa vikundi na taasisi. Baada ya hapo unalipa kwa siku kulingana na kifurushi chako.
Angalia beiMweka hazina, mwenyekiti na katibu wanaweza kuendelea kurekodi michango, marejesho na mahudhurio hata bila mtandao. Kazi zinahifadhiwa kwenye simu na kutumwa zenyewe mtandao ukirudi.
Fungua Kazi bila mtandao mara moja. Orodha ya wanachama, aina za michango na mikopo inahifadhiwa kwenye simu yako.
Mtandao ukikatika, weka mchango, marejesho au mahudhurio. Kila kazi inaingia kwenye foleni ya kutuma.
Kazi zinatumwa kiotomatiki, mara moja tu kila moja, na risiti rasmi inatolewa na seva.
Mweka hazina anarekodi hisa, akiba na michango mingine bila mtandao.
Malipo ya mikopo yanarekodiwa shambani au sokoni, na baki inasasishwa yakitumwa.
Mwenyekiti au katibu anaweka waliohudhuria; faini ya kutokuja inawekwa na mfumo.
Kazi ikitumwa mara mbili kwa bahati mbaya, mfumo unaipokea mara moja tu.
Ukitoka (Toka), data ya offline inafutwa. Kuna pia kitufe cha kufuta data ya kifaa.
Teller na afisa wa mikopo wanapokea marejesho na kurekodi ziara bila mtandao.
Anza kutumia VisaMi ndani ya dakika chache.
Unda akaunti kwa dakika chache: jina la kikundi, aina ya kikundi (VICOBA, Kikundi Kidogo au Umoja), eneo na msimamizi.
Sajili wanachama wote. Kila mwanachama anaweza kuingia na kuona taarifa zake mwenyewe.
Rekodi michango, idhinisha mikopo (VICOBA), panga mikutano na fuatilia fedha zote na ripoti kwa urahisi.
Mfumo huu umejengwa kwa ajili ya kila mwanachama wa kikundi na kila mfanyakazi wa taasisi, na uwezo tofauti kwa kila jukumu.
Anasimamia taasisi nzima: matawi, watumiaji, hesabu za fedha na idhini kuu.
Anasimamia tawi lake: wafanyakazi, mikopo na fedha za kaunta.
Anafanya kazi na wateja: usajili, maombi ya mikopo na ufuatiliaji wa marejesho.
Anashughulikia fedha taslimu za kaunta: marejesho, kutoa mikopo na kufunga siku.
Ana udhibiti kamili wa kikundi — anaona kila kitu na anaweza kuidhinisha maamuzi yote ya fedha.
Anashughulikia kumbukumbu za kikundi — anarekodi michango, mikutano na matukio yote ya kila siku.
Anaona taarifa zake mwenyewe tu — michango yake, mikopo yake, na hali yake ya sasa ndani ya kikundi.
Soma mwongozo wa hatua kwa hatua, kisha angalia majibu ya maswali ya kawaida.
VisaMi = VIcoba + SAving + MIcrofinance. Jina kamili ni VisaMi Financial Technology: jukwaa la kidijitali kutoka Moescience kwa VICOBA, vikundi vya akiba na mikopo, na taasisi za microfinance.
Bonyeza “Sajili kikundi”, jaza taarifa za kikundi, kisha ongeza wanachama na uanze kurekodi michango na mikopo. Mwongozo unaeleza kila hatua.
VICOBA ni kwa vikundi vinavyokopeshana na kuweka akiba kati ya wanachama wenyewe. Microfinance ni kwa taasisi inayotoa mikopo kwa wateja kupitia matawi na wafanyakazi wenye majukumu tofauti.
Taasisi huandaliwa na timu yetu: tunaweka jina rasmi la taasisi, matawi na wasimamizi wawili. Wasiliana nasi kwa WhatsApp au simu. Baada ya hapo wafanyakazi huingia kupitia kiungo cha “Wafanyakazi: Ingia”.
Kupitia ukurasa wa kuingia wa wafanyakazi wa microfinance (kitufe cha “Ingia (MFI)” juu ya ukurasa huu). Ni tofauti na kuingia kwa wanachama wa VICOBA.
Ndiyo. Mweka hazina anaweza kurekodi michango na marejesho ya mikopo, na mwenyekiti au katibu mahudhurio, hata mtandao ukikatika. Kazi zinahifadhiwa kwenye simu na kutumwa zenyewe mtandao ukirudi, mara moja tu kila moja. Ili ifanye kazi, fungua “Kazi bila mtandao” mara moja ukiwa na mtandao. Mikopo mipya, idhini na ripoti za mwisho hubaki mtandaoni kwa usalama.
Siku 90 za kwanza ni bure. Kikiisha, watumiaji wanaona ukurasa wa “Kifurushi kimeisha” na hawawezi kuendelea kufanya kazi hadi ulipe. Data yako haipotei. Ukilipa na kuwasiliana nasi, akaunti inafunguliwa tena.
Ndiyo. Unaweza kuchagua marejesho ya kila siku (siku 26 kwa mwezi, bila Jumapili), kila wiki (wiki 4 kwa mwezi) au kila mwezi. Mfumo unahesabu ratiba na kiasi cha kila malipo.
Piga au tuma WhatsApp kwa +255 768 139 301, au tuandikie moescience@proton.me.
Bei zote zinahesabiwa kwa siku. Andika siku unazotaka kulipia (kima cha chini siku 7) na uone jumla papo hapo.
Una swali kuhusu kifurushi, usajili au kuhamisha data? Tuandikie au tupigie — tutakujibu haraka.
Vikundi hujisajili wenyewe na kuanza mara moja. Taasisi huandaliwa na timu yetu baada ya ombi. Miezi 3 bure kwa wateja wapya.